Shirika la habari la Ahlubayt (as):
Rais wa Iraq Bw Barham Salih ameweka wazi kwamba kiongozi mkuu wa kidini nchini humo ni sababu asilia ya Iraq kuwepo katika hali ya amani na utulivu.
Hayo ameyaweka wazi katika hotuba yake ailiyoitoa katika kongamano kubwa la kiuchumi duniani huko Davos nchini Uswisi.
Aidha pia katika hotuba yake hiyo Rais Barham ameweka wazi kwamba uwepo wa uchaguzi wa haraka wa Bunge la nchi yake hiyo ni fursa makini sana katika kuhakikisha kwamba wanatatua mizozo mbalimbali ya kisiasa nchini humo.
Pia Rais Barham ameelezea hatua ya hukumu ya nchi yake kuyataka majeshi ya ajnabi kuondoka nchini Iraq na kusema kwamba ni kutokana na kila ambacho wananchi wamehisi kuwa uwepo wa majeshi hayo ulikuwa ni udhalili na kutoipa heshima Dola ya Iraq, jambo ambalo linatakiwa kuwepo ili kuhakikisha uthabiti na uwepo wa nguvu katika Mashariki ya kati.
Kujitolea kwa majeshi ya nchi, vikundi vya kimgambo vya wananchi, ni katika mambo ambayo kwa kiwango kikubwa mo yaliyochangia kumalizana na tatizo la Daesh nchini humo kwa mujibu wa Rais Barham.
Katika kujibu swali aliloulizwa juu ya Iran kuingia Iraq hasa baada ya Majeshi ya Marekani kutoka alisema kuwa Iraq na Iran ni majirani wa karibu mno, na siku zote ujirani wao una nafasi kubwa mno, hasa ukizingatia mataifa haya miaka mingi mno yalikuwa katika vita na mapigano lakini leo hii hakuna hata mwananchi mmoja anayeomba hali ile irudi tena.
Pia Rais Barham ameweka wazi kutambua kwake mchango wa Shahidi Qasem Suleimani katika kupambana na Daesh na kusema kuwa kwa hakika alikuwa ni mfano wa kuigwa katika mambo ya usalama wa taifa la Iraq, kama ambavyo alishirikiana bega kwa bega na majeshi ya nchi hiyo kupambana.